Jeremiah 5:9-29

9 aJe, nisiwaadhibu kwa ajili ya hili?”
asema Bwana.
“Je, nisijilipizie kisasi
juu ya taifa kama hili?

10 b“Piteni katika mashamba yake ya mizabibu na kuyaharibu,
lakini msiangamize kabisa.
Pogoeni matawi yake,
kwa kuwa watu hawa sio wa Bwana.
11 cNyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda
wamekuwa si waaminifu kwangu kamwe,”
asema Bwana.

12 dWamedanganya kuhusu Bwana.
Wamesema, “Yeye hatafanya jambo lolote!
Hakuna dhara litakalotupata;
kamwe hatutaona upanga wala njaa.
13 eManabii ni upepo tu, wala neno halimo ndani yao,
kwa hiyo hayo wayasemayo na yatendeke kwao.”
14 fKwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote:

“Kwa sababu watu hawa wamesema maneno haya,
nitayafanya maneno yangu vinywani mwenu kuwa moto,
na watu hawa wawe kuni
zinazoliwa na huo moto.
15 gEe nyumba ya Israeli,” asema Bwana,
“Ninaleta taifa toka mbali dhidi yako,
taifa la kale na linaloendelea kudumu,
taifa ambalo lugha yao huijui,
wala msemo wao huwezi kuuelewa.
16 hPodo zao ni kama kaburi lililo wazi,
wote ni mashujaa hodari wa vita.
17 iWatayaangamiza mazao yenu na chakula chenu,
wataangamiza wana wenu na mabinti zenu;
wataangamiza makundi yenu ya kondoo na ya ngʼombe,
wataangamiza mizabibu yenu na mitini yenu.
Kwa upanga wataangamiza
miji yenye maboma mliyoitumainia.
18“Hata hivyo katika siku hizo, sitakuangamiza kabisa,” asema Bwana. 19 j“Nao watu watakapouliza, ‘Kwa nini Bwana, Mungu wetu ametufanyia mambo haya yote?’ utawaambia, ‘Kama vile mlivyoniacha mimi na kutumikia miungu migeni katika nchi yenu wenyewe, ndivyo sasa mtakavyowatumikia wageni katika nchi ambayo si yenu.’

20“Itangazie nyumba ya Yakobo hili
na ulipigie mbiu katika Yuda:
21 kSikieni hili, enyi watu wapumbavu, msio na akili,
mlio na macho lakini hamwoni,
mlio na masikio lakini hamsikii:
22 lJe, haiwapasi kuniogopa mimi?” asema Bwana.
“Je, haiwapasi kutetemeka mbele zangu?
Niliufanya mchanga kuwa mpaka wa bahari,
kizuizi cha milele ambacho haiwezi kupita.
Mawimbi yanaweza kuumuka, lakini hayawezi kuupita;
yanaweza kunguruma, lakini hayawezi kuuvuka.
23 mLakini watu hawa wana mioyo ya ukaidi na ya uasi,
wamegeukia mbali na kwenda zao.
24 nWao hawaambiani wenyewe,
‘Sisi na tumwogope Bwana Mungu wetu,
anayetupatia mvua za masika na za vuli kwa majira yake,
anayetuhakikishia majuma ya mavuno kwa utaratibu.’
25Matendo yenu mabaya yamezuia haya yote,
dhambi zenu zimewazuia msipate mema.

26 o“Miongoni mwa watu wangu wamo walio waovu
wanaovizia kama watu wanaotega ndege,
na kama wale wanaoweka mitego
kuwakamata watu.
27Kama vitundu vilivyojaa ndege,
nyumba zao zimejaa udanganyifu;
wamekuwa matajiri na wenye nguvu,
28 pwamenenepa na kunawiri.
Matendo yao maovu hayana kikomo;
hawatetei mashauri ya yatima wapate kushinda,
hawatetei haki za maskini.
29Je, nisiwaadhibu kwa ajili ya hili?”
asema Bwana.
“Je, nisijilipizie kisasi
juu ya taifa kama hili?
Copyright information for SwhNEN